Je, ni kweli 5G ina madhara kwa Binaadamu?

Watu wengi wamekuwa wakisoma habari na kusikia kuwa 5G network ina madhara makubwa kwa binaadamu, tuangalie hili.

Kwanza tuanze kwa kuielewa 5G.

3G na 4G networks ndio zipo katika nchi yetu hivi sasa (wakati naandika hii makala). Na tunajua jinsi gani 3G na 4G zilivo na kasi. Kutoka 3G kwenda 4G ilikuwa ni maboresho ya spidi ya internet. Japokuwa 5G pia ni maboresho ya spidi, lakini hii ni zaidi ya spidi tu ya internet ni kwa sababu itakuwa inatumia masafa ya 1Ghz – 86 Ghz.

5G itakuwa inatumia mfumo mpya wa usafirishaji DATA na ambao utakuwa wa haraka sana, mfumo huo unaitwa Millimeter Wave. Mawimbi yake yanaathiriwa na kuta nene, mvua na hata maji ya mwili ndani ya binaadamu yanaweza kuwa kikwazo cha uwezo wa mtandao huo.

This image has an empty alt attribute; its file name is network-4892118_640.jpg
5G itatumika katika TV, Kompyuta, Simu, Tablet, Magari yanayojiendesha wenyewe, taa za kuongoza barabarani n.k

Ili kuwezesha huduma hio kupatikana, kutahitajika uwepo wa antenna nyingi kiasi kwamba kila baada ya mita 250 kutawekwa antenna. Antenna za 5G hazitokuwa kubwa kama zile za 3G na 4G, antenna zake zitakuwa ndogo zaidi. Antenna hizi zitatumika kama kituo cha kurudia signals ambazo zinatumwa na mnara mkuu ulioko katika eneo husika.

5G itakuwa inatumia teknolojia inayoitwa Beamforming. Badala ya mawimbi kurushwa ovyo ovyo, teknolojia hio itakuwa inarusha mawimbi yake moja kwa moja kwa kifaa chako. Kwa sababu ya uwepo antenna sehemu tofauti, mtandao huo utawezesha kujua kifaa chako kiko wapi kwa usahihi zaidi na kuyarusha mawimbi hayo moja kwa moja.

This image has an empty alt attribute; its file name is car-4343633_640.jpg
Gari zitakuwa zinawasiliana pamoja na vifaa vyengine vitakavotumia mtandao wa 5G

Kupeleka mawimbi hayo na kuwezesha kuepuka vikwazo, maelfu ya antenna zitahitajika, katika jiji la New York Marekani, inakisiwa kuwa antenna 10,000 zitahitajika ili kuwezesha upatikanaji wa mtandao huo. Hii ina maana kuweka mtandao wa 5G itakuwa ghali sana. Kwa sababu ni ghali, baadhi ya miji na vijijini wanaweza kuachwa nyuma kwa miaka mingi ikiwa makampuni ya mitandao ya simu ikiamua kuweka 5G. Na hasa ukizingatia kuwa 4G kwa sasa bado haijaenea vizuri nchini kote, na pia spidi yake kamili kuwa bado haijafikiwa.

Mtandao wa 5G utakuwa na uwezo wa kupakua kitu kutoka mtandaoni kwa spidi ya 100Mbps hadi 4Gbps, unaweza kupakua movie kwa dakika chache sana. Lakini kitu kikubwa kuhusu 5G sio spidi tu, bali ni kitu kinaitwa Latency. Latency ni muda ambao vifaa viwili huchukua kuwasiliana, na 5G itawezesha hilo kwa kiwango cha chini 1 milliseconds. Yaani ukiwa unaingia kwenye mtandao na kuandika website uitakayo na kubofya ENTER, kawaida huwa kuna muda mchache ambao unasubiria tovuti hio kutokea, lakini kwa mtandao wa 5G, hakutakuwa na muda wa kusubiri na hapo hapo tovuti hio itatokea (kama hakuna tatizo na seva zilizohifadhi hio tovuti).

Hapa ndio utaona umuhimu wa 5G kuwa ni zaidi ya kutizama facebook, instagram na nyenginezo. Mtandao huu utawezesha magari kuwasiliana yakiwa barabarani na kupunguza ama kuepuka ajali. Hii ikiwa gari hizo zote zinatumia mtandao huo. Hadi taa za kuongoza magari zitaweza kutumia mtandao huu na pale inapoona kuwa kuna dereva anakuja kwa kasi na kuwa anapuuzia alama za barabarani, na gari yake inatumia mtandao wa 5G na yako pia, basi utapata taarifa kuhusu dereva huyo anavoendesha, na wewe kama dereva kuchukua tahadhari au hata gari yako mwenyewe yaweza kupiga breki na kuepusha ajali kutokea eneo hilo na taa za muongozo zitawaka nyekundu kuashiria usipite. Yapo mengi sana ambayo 5G yanaweza kufanikisha.

This image has an empty alt attribute; its file name is technology-4816658_640.jpg

Je ina madhara kwa binaadamu?

Kuna watu wanasema kuwa 5G ina madhara katika mwili wa binaadamu na wengine wamefikia kusema kuwa inatumika katika kudhoofisha kinga ya mwili. Mionzi ni hatari kwa mwili wa binadaamu, katika miaka ya 2000 simu zilianza kutiliwa shaka kuwa zina madhara na kuweza kusababisha kensa ya ubongo. Lakini hadi sasa hakuna ushahidi wenye kuonesha kuwa ongezeko la kensa kwa binaadamu limechangiwa na matumizi ya simu.

Hata hivyo mionzi ya 4G ni dhaifu sana kusababisha matatizo kwa binaadamu na kufikia kuharibu seli za mwili. Lakini 5G, ina uwezo mkubwa zaidi kuliko 4G, inakaribia na microwave oven ya nyumbani. Vile vile baadhi ya wanasayansi wamekuwa na wasiwasi katika matumizi ya 5G kwa kuamini kuwa inaweza kutumika na vyombo vya dola kwenye maandamano, kama vile kuiwasha na kuongeza nguvu kwa na kusababisha waandamanaji kuhisi joto kali sana lenye kuunguza katika mwili.

Kwa sasa hakuna ukweli kamili na hasa ukizingatia kuwa ni teknolojia mpya. Japokuwa 5G ina uwezo kama mionzi ya microwave oven, lakini microwave hio nguvu yake imekuwa inadhibitiwa katika sehemu ndogo wakati 5G itakuwa nje ambapo hali ya hewa itaifanya mionzi hio kutotoa joto kama litolewalo na oven. Chukulia kama vile microwave umeiacha wazi nje kwenye veranda, mpita njia hatohisi mabadiliko yoyote kwa sababu umoto unaotolewa na hilo oven, unapotea kwenye hewa ilioko nje.

Uchambuzi wa muangaza ni mkali sana kuliko microwave na bado athari yake ni ndogo kwa mwili wa binaadamu. Kwa sababu ya kutumia masafa makubwa haimaanishi kuwa ina nguvu kubwa ya kumuathiri binaadamu. Baadhi ya wanasayansi wanasema ili 5G iwe na athari kwa binaadamu, basi itatakiwa izidishwe nguvu zaidi ya mara elfu ya nguvu iliokuwa nayo sasa. Na kuhusu swali la kensa, kwa taaluma ilioko sasa kuhusu mionzi na mawimbi, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya teknolojia ya 5G.

Sio kila mionzi ni hatari kwa afya ya binaadamu. Kwa kumalizia, tunaweza kusema kuwa teknolojia ya 5G ni salama kwa matumizi ya binaadamu na italeta mapinduzi katika upande mzima wa teknolojia.

Share on facebook
Facebook
Share on google
Google+
Share on twitter
Twitter
Share on linkedin
LinkedIn